Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi Kavu na Majini SUMATRA Mkoani Tabora imawaomba viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kuisadia serikali kuwaelimisha wananchi kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuweza kupunguza ajali mkoani humo

Ombi hilo limetolewa na Afisa mfawidhi wa mamlaka hiyo mkoani Tabora bwana Joseph Maiko wakati akizungumza na East Radio Ofisini kwake.

Amesema viongozi wa dini wanakutana na watu wengi katika nyumba zao za ibada hivyo ni vyema kuisaidia serikali kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza tatizo la ajali mkoani humo.

Aidha Bw. Maiko ameongeza kuwa watumiaji wengi wa vyombo vya moto bado hawazingatii sheria za usalama barabarani na hivyo kuwepo kwa ajali nyingi zisizotarajiwa mkoani humo.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa madhebu ya dini mkoani humo Shekhe Ramadhani Rashidi Juma amesema wao kama viongozi wa dini wamepokea ombi hilo na kuahadi kushirikiana na serikali katika kupunguza tatizo la ajali mkoani humo.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: