Saturday, 5 May 2018

SIMBA KUPIGA ZOEZI LA MWISHO KWA AJILI YA NDANDA KESHO


Na George Mganga

Kikosi cha Simba kinafanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Ndanda utakaopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kesho Jumamosi.

Simba inafanya mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Boko Veterani uliopo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.

Taarifa kutoka kambini zinasema kuwa hali ya wachezaji kiafya iko vizuri na hakuna aliye majeruhi hivi sasa.

Simba itakuwa inaingia kukabiliana na Ndanda ikiwa na kumbukumbu ya ushindi dhidi ya Yanga wa bao 1-0 Jumapili ya wiki jana.

No comments:

Post a Comment