Mashindano ya shule za sekondari ya Copa Umisseta, yalizinduliwa Zanzibar kwa shamrashamra mbalimbali za michezo na burudani katika uwanja wa Aman na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali,wadau wa michezo na wanafunzi wa shule za sekondari na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud. 

 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, alisema suala la michezo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalipa kipaumbele kikubwa kwa kuwa inaamini kuwa inayo faida nyingi baadhi yake ikiwa ni kujenga afya,kuleta umoja,burudani na inazo fursa kubwa za ajira hususani kwa vijana na aliipongeza kampuni ya Coca-Cola kwa kuwa mstari wa mbele kudhamini mashindano haya. ZNZ%2BPHOTO%2B1 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Ayoub Mohamed Mahmod akipokea zawadi ya mpira wa kufanyia mazoezi kutoka Coca-Cola baada ya hafla ya uzinduzi. ZNZ%2BPHOTO%2B2 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Maghribi, Ayoub Mohamed Mahmod (wa tatu kulia) akikabidhi jezi na mpira kwa mwalimu Mussa Abdi Khamis wa shule ya sekondari ya penae. ZNZ%2BPHOTO%2B3 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud, akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa mashindano ya Copa UMISSETA. ZNZ%2BPHOTO%2B4 Moja ya timu ikikaguliwa wakati wa uzinduzi huo. PHOTO%2BZNZ%2B6 Wananchi wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: