Tuesday, 29 May 2018

Serikali kuwafikisha Mahakamani na kuwafutia hati ya umiliki ardhi Wananchi hawaWaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema serikali itawafikisha Mahakamani na kuwafutia hati ya umiliki wananchi wote wanaomiliki ardhi ambao wamekuwa hawalipi kodi ya ardhi.

Waziri Lukuvi ametoa kauli hiyo leo Mei 29, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 37 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/219 na kusema katika mwaka huu wa fedha ambao unaishia mwezi Juni Wizara ya Ardhiilipanga kukusanya Bilioni 112.5 vinavyotokana na vyanzo vya mapato ya kodi, ada na tozo mbalimbali za ardhi lakini hadi Mei 15 wizara imeshakusanya Bilioni 78.9 sawa na asilimia 70 ya lengo lililokusudiwa.

"Natoa onyo kwa wadaiwa sugu wote wasiolipa kodi ya pango la ardhi kwamba serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani, kuitaifisha mali zao ili kufidia kiwango cha kodi wanachodaiwa au kufutiwa hati miliki", amesema Lukuvi.

Pamoja na hayo, Waziri Lukuvi ameendelea kwa kusema "kwa hiyo natoa wito kwa wote wanaomiliki ardhi kisheria wakumbuke kulipa kwa mujibu wa sheria".

Kwa upande mwingine, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema bado kuna muitikio mdogo wa wananchi kumilikishwa ardhi hususan katika maeneo ya urasimishaji ambayo yapo skwakta

No comments:

Post a comment