Friday, 11 May 2018

SAMATTA AIOKOA GENK KUPATWA NA KIPIGOKikosi cha KRC Genk jana anachocheza Mtanzania, Mbwana Samatta, jana kilikwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya KAA Gent katika mchezo wa Play Offs kwenye ligi ya Ubelgiji.

Samatta aliingia Uwanjani dakika ya 54 ya mchezo akitokea benchi kuchukua nafasi ya Mgiriki Nikolaos Karelia wakati timu yake ikiwa nyuma kwa bao 1-0.

Baada ya Samatta kuingia Uwanjani, ilimchukua takribani dakika 12 kuisawazishia Genk katika dakika ya 66 ya mchezo na mechi hiyo mpaka inamalizika matokeo yalikuwa ni 1-1.

Matokeo hayo yameifanya Genk kufikia jumla ya pointi 32 ikiwa imecheza jumla ya mechi 8 ikikamata nafasi ya 6.

No comments:

Post a Comment