Sunday, 27 May 2018

SALAH AFANYA MAAMUZI JUU YA REAL MADRID BAADA YA KUCHEZEWA RAFU MBAYA NA RAMOSMshambuliaji wa kimataifa wa Liverpool, Mmisri, Mohammed Salah, amesema hatoweza kujiunga na Real Madrid kutokana na mchezo ambao si wa kiungwana waliouonesha jana wakati wakicheza mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Ukraine.

Salah ameeleza kusikitishwa zaidi na tukio la nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos kwa kitendo chake cha kumuumiza mkono na kupelekea kuondolewa nje ya Uwanja baada ya kushindwa kuhimili maumivu.

Mchezaji huyo amesema kitendo kama hicho ni mbinu chafu za kujitafutia matokeo badala ya kucheza mpira ambao unafuata sheria zote 17 za mchezo wa soka.

Kuafuatia rafu iliyopelekea kuumia mkono wake, Salah amesema hataweza kujiunga na timu hiyo ambayo imeonesha nia ya dhati kutaka kumsajili hivyo ataendelea kusalia Liverpool na si kwenda Madrid.

Katika mchezo huo uliopigwa mjini Kiev, ulimalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kuweza kubeba taji la tatu mfululizo katika UEFA Champions League.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: