Thursday, 3 May 2018

RUFAA YA YANGA KUHUSIANA NA MBEYA CITY KUZIDI UWANJANI, MAJIBU KUTOKA LEOAfisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura, atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari za Michezo Saa 6:00 mchana Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kikao hicho kinatarajiwa kutoa majibu ya rufaa ya Yanga waliyokata wakieleza wachezaji wa Mbeya City kuzidi Uwanjani katika mchezo dhidi yao uliopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mbali na rufaa hiyo, Mbeya City nao walikata rufaa ya kudai Mshambuliaji wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa, awajabishwe baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wao kwenye mchezo huo.

Mbali na Chirwa, Mbeya City pia walipinga faulo aliyochezewa mahadhi na kuzaa bao la Yanga lillofungwa na Raphael Daud kuwa haikuwa halali wakida kuwa Mahadhi alijiangusha.

Mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ilimalizika kwa sare ya bao 1-1.

No comments:

Post a Comment