Wednesday, 2 May 2018

RC Mongella aagiza kampuni za ulinzi kuhakikiwa

Na James Timber, Mwanza
Kampuni za Ulinzi katika Mkoa wa Mwanza zimetakiwa kuhakikiwa kabla ya mwezi wa sita mwaka huu kutokana na baadhi ya kampuni kumiliki silaha pasipo kandarasi ya ulinzi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella  katika Siku ya Mei Mosi alisema kesi za kampuni hizo zimekuwa ni nyingi jambo linalotishia usalama wa raia na mali zao.

"Naagiza Mkuu wa Polisi, Kamati za Ulinzi na Usalama na Mshauri wa Mgambo Mkoa waanze zoezi la kuhakiki kampuni hizo mpaka 30, June Mwaka huu wawe wameleta majibu ya kutosha.

Aidha Mongella alisema atahakikisha anatatua changamoto ambapo watu wanatumikishwa bila kupewa haki zao za msingi katika kampuni hizo jambo linalodhorotesha ukuaji wa uchumi

No comments:

Post a Comment