Msanii wa uziki kutoka WCB  , Rayvanny amefunguka na kueleze kwa undani kwanini msanii Rosa Ree ndio msanii pekee wa kike katika remix ya wimbo wake wa Pochi nene.

Rayvanny anasema kuwa amekuwa akivutiwa sana na muziki wa Rosa Ree na pia katika wimbo huu rapper pekee ambaye angeweza ku-fit kutokana na wimbo ulivyo , alikuwa ni Rosa Ree na sio mwingine

“Nawakubali wasichana wote wanaorap lakini Rosa Ree is my favorite wangu naweza kusema lakini niliona kama atafaa zaidi kutokana na concept ya wimbo wenyewe,” amesema.

“Ukimsikia anavyo-sound kama Nicki Minaj sio Nicki Minaj, nikaona kwenye biti kama lile ataleta vibe na ndio maana nikaamua kumuweka,” Rayvannuy ameiambia Wasafi TV.
Katika remix ya wimbo huo watakuwepo wasanii Khaligraph Jones, Godzilla, Rosa Ree, Izzo Bizness, Country Boy, Young Dee na Wakorinto.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: