Friday, 4 May 2018

RAIS MAGUFULI AMPIGIA SIMU PROF. KITILA MBELE YA WANANCHI, ‘ATUMBUA JIPU’


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amempigia simu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu kero ya maji katika eneo la Kidodi Morogoro. JPM amemtaka Prof. Kitila afike eneo hilo mara moja kushughulikia kero hiyo.

Aidha, Rais Magufuli ameagiza Mkandarasi wa Maji Kata ya Kidodi, akamatwe mara moja kwa kushindwa kukamilisha mradi wa maji ndani ya wakati uliopo kwenye makubaliano ya utekelezaji wa mradi huo.

“Ninafahamu kuna mradi wa maji wa Tsh. Milioni 800, mkandarasi alipewa lakini mpaka sasa maji hayajafika kwa wananchi, nilidhani mbunge wenu atauliza achukuliwe hatua gani lakini hajauliza, sasa mkandarasi kama alikula hela atazitapika, naomba mumfikishie huu ujumbe,” alisema Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment