Friday, 4 May 2018

Rais Magufuli ahani msiba wa Kandoro Iringa


Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wamehani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Marehemu Mzee Abbas Kandoro katika eneo la Ihema nje kidogo ya Mji wa Iringa.

Kandoro aliaga dunia usiku wa Aprili 28, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

Mwili wa marehemu Kandoro uliagwa kesho yake kwenye Msikiti wa Manyema uliopo Kariakoo baada ya kuswaliwa kisha kupelekwa nyumbani kwake Mbweni Luis utakapoagwa tena na baadaye kusafirishwa kwenda Kijijini Ihemi mkoani Iringa kwa mazishi ambayo yalifanyika Jumapili, Aprili 30, 2018.


Abbas Kandoro aliwahi kushika nafasi ya ukuu wa mkoa katika zaidi ya mikoa sita Tanzania Bara ikiwemo Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Singida na Mbeya.

No comments:

Post a Comment