Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta leo Mei 16, 2018 amesaini muswada wa matumizi mabaya ya Kompyuta na makosa ya mtandao na kuwa sheria rasmi ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu nchini humo.
Maamuzi hayo ya Kenyatta yamefanyika Ikulu jijini Nairobi mbele ya Makamu wake William Ruto, ambapo wamesema kuwa hatua hiyo itapunguza kama sio kukomesha vitendo vya uhalifu kwenye mitandao ya kijamii.

Sheria hiyo pia itahusisha na waandishi wa habari ambao wataandika habari FEKI ambapo kosa hilo litajumuishwa kwenye baadhi ya vipengele vya makosa ya uhalifu mtandao.
Hatua hiyo ya Kenya inakuja ikiwa ni miaka miwili tangu aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho mwaka 2015 kusaini muswada wa sheria ya makosa ya mtandao.
Hata hivyo, Waandishi wa Habari na wanaharakati nchini Kenya wamepinga hatua hiyo ya Rais Kenyatta kwa kudai kuwa hatua hiyo ni kandamizi na inakiuka haki za binadamu
Share To:

msumbanews

Post A Comment: