Tuesday, 29 May 2018

PROFESA MDOE ASHIRIKI KONGAMANO LA SAYANSI NA TEKNOLOJIA NCHINI ISRAELNaibu Katibu Mkuu Profesa James Mdoe yuko mjini Jerusalem nchini Israel, kwa ajili ya kushiriki kongamano la Mawaziri la kuadhimisha miaka 70 ya Sayansi na Teknolojia katika kuhudumia wanadamu.

 Mkutano huo ulioanza jana ulifungukiwa rasmi na Waziri Mkuu wa Israel ambapo Mada kuu ya mkutano huo ni “kufikiria nje ya boksi”.

Kongamano hilo la siku 4 linawashirikisha Mawaziri, Naibu Mawaziri na viongozi mbalimbali.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
29/05/2018
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Application yetu bonyeza hapo chini

Tumekurahisishia; No comments:

Post a comment