Wednesday, 2 May 2018

PICHA : REAL MADRID YATINGA FAINALI ULAYA KWA MABAO 4-3

  WABABE wa soka la Ulaya, Real Madrid wametinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya tatu mfululizo na ni mara ya nne ndani ya misimu mitano iliyopita baada ya kuiondoa Bayern Munich katika nusu fainali.


Real Madrid imetimiza lengo hilo licha ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bayern, usiku wa jana ambapo jumla wanakuwa wametinga fainali kwa mabao 4-3 kutokana na kushinda 2-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa Munich, Ujerumani, wiki iliyopita.

Bayern ambayo iliuanza mchezo huo kwa kasi na kupata bao la haraka dakika ya sita kupitia kwa Joshua Kimmich, ilijikuta ikikosa nafasi kadhaa za wazi na hivyo kuwafanya wenyeji waliokuwa ndani ya Uwanja wa Santiago Bernabeu kutulia na kuanza kumiliki mpira.

Dakika ya 11, Karim Benzema alifunga bao la kichwa akipokea krosi ya Marcelo na kufanya mchezo kuwa mgumu kwa Bayern ambao ni mabingwa wa Bundesliga.

Kosa lililofanywa na kipa wa Bayern, Sven Ulreich aliporudishiwa mpira na kuteleza, kulimfanya Benzema kuwa na kazi nyepesi ya kufunga bao la pili katika dakika ya 46 na hivyo kuwamaliza nguvu Bayern.

Akiichezea Bayern kwa mkopo kutoka Real Madrid, James Rodriguez alifunga bao la kusawazisha kwa shuti kali dakika ya 63 kufanya matokeo kuwa 2-2 lakini hakushangilia bao lake hilo, matokeo ambayo yalidumu hadi mwisho wa mchezo huku staa wa Madrid, Cristiano Ronaldo akitoka bila bao kwa mechi ya pili mfululizo licha ya kuwa yeye ndiye kinara wa mabao kwenye michuano hiyo.

Hivyo, sasa Real Madrid ambayo imeshatwaa kombe hilo mara 12 inasubiri mshindi wa mchezo wa Roma dhidi ya bingwa mara tano wa kombe hilo, Liverpool, ambazo zinatarajiwa kukutana leo katika nusu fainali ya pili, Liverpool ikiwa mbele kwa mabao 5-2. Fainali ya mwaka huu itapigwa kwenye Uwanja wa NSC Olimpiyskiy jijini Kiev, Ukraine Jumamosi ya Mei 26

REAL MADRID (4-4-2):

Navas 9; Vazquez 6, Varane 6, Sergio Ramos 6, Marcelo 7; Kovacic (Casemiro 73min, 6), Kroos 6, Modric 7, Asensio 6 (Nacho 88); Benzema 7 (Bale 72, 6), Ronaldo 6
Subs not used: Casilla, Ceballos Fernandez, Hernandez, Mayoral
Goals: Benzema 11, 46
Bookings: Modric, Lucas, Casemiro, Varane
Manager: Zinedine Zidane 7

BAYERN MUNICH (4-2-3-1):

Ulreich 5; Kimmich 7, Hummels 7, Sule 6, Alaba 7; Tolisso 6 (Wagner 76), Thiago 6; Muller 6, Rodriguez 8 (Javi Martinez 84), Ribery 6; Lewandowski 6
Subs not used: Starke, Rafinha, Mai, Dorsch, Rudy
Goals: Kimmich 3, Rodriguez 63
Booked: None

Manager: Jupp Heynckes 6
Referee: Cuneyt Cakir (Turkey) 7
Att: 77,459

No comments:

Post a Comment