Friday, 18 May 2018

Nina uwezo wa kutoa nyimbo kila siku/mwezi lakini nitafilisika – Alikiba

Msanii Alikiba amefunguka kwanini hapendelei kutoa nyimbo kila mara.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Mvumo wa Radi’, katika mahojiano na Planet Bongo ya East Africa Radio amesema kuwa muziki ni biashara na kila biashara huwa na msimu wake.
Ameendelea kwa kusema hadi muziki unamaliza mwaka masikioni mwa watu ni kwamba una miguu mirefu, yaani muziki wake unaishi lakini haimaanishi kuwa hana uwezo wa kutoa nyimbo kila wakati.
“Na vile vile nina uwezo wa kutoa nyimbo kila siku, mwezi mzima nina uwezo wa kutoa nyimbo lakini nitajitia hasara, nitafilisika,” amesema Alikiba.
Alikiba kwa sasa anatamba na ngoma mpya ‘Mvumo wa Radi’, ikiwa ni zaidi ya miezi nane imepita tangu alipotoa ngoma inayofahamika kama Seduce Me.

No comments:

Post a comment