Rapa Nikki wa Pili ametoa wito kwa wasanii wa muziki nchini wasusie kusherehekea maadhimisho ya sikukuu ya Mei Mosi kwani siku hiyo haina tija katika kazi zao za muziki.
Nikki wa Pili
Nikki amesema wasanii wamekosa ulinzi wa kisheria kiasi kwamba hata wakipatwa na majanga kwenye maeneo yao ya kazi hawana pa kwenda kushtaki wala kulalamika hivyo ni bora wakabaki kimya na kufanya kazi nyingine lakini sio kupoteza muda na Mei Mosi.
Ikiwa leo siku ya wafanyakazi, wasanii haituhusu kwakuwa hatuna ulinzi wa kisheria/taratibu tuwapo maeneo yetu ya kazi, hata ukishika mic ina shot, au steji mbovu ukaanguka, au avamiwe au apigwe na kitu jukwaani kutakuwa na malipo au fidia yoyote? hapana kwakuwa halindwi na sheria za kazi awapo kazini kwake. Ndugu msanii pambana na hali yako na uzingatie maadili“ameandika Nikki wa Pili kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Nikki wa Pili ni moja ya wasanii ambao hawaamini katika maisha ya kuajiriwa kwani anaamini ni utumwa hii ni kwa mujibu wa maelezo anayoyatoa juu ya wimbo wake wa Sitaki Kazi.
Leo Mei 01, 2018 ni siku ya Wafanyakazi duniani maarufu kama (Mei mosi) ambapo kitaifa imeadhimishwa mkoani Iringa na mgeni rasmi alikuwa ni Rais Magufuli.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: