Wednesday, 23 May 2018

NDANDA KUJIKWAMUA KUSHUKA DARAJA LEO NANGWANDA SIJAONA


Ligi Kuu Soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja ambapo Ndanda FC watakuwa nyumbani Nangwanda Sijaona kucheza na Mwadui FC ya Shinyanga.

Ndanda inayopigania kuepuka kushuka daraja itakuwa inapigania kupata alama tatu muhimu ili kujitengenezea mazingira ya kusalia kwenye ligi.

Timu hiyo ipo nafasi ya 15 imekuwa imejikusanyia alama 23 na chini yake akiwepo Njombe Mji FC aliye na alama 22.

Ndanda na Njombe Mji ndizo timu pekee zilizo kwenye mazingira hatarishi zaidi kushuka daraja msimu huu endapo matokeo yao kwenye michezo iliyosalia yatazidi kuwa mabaya.

No comments:

Post a Comment