Monday, 14 May 2018

Naibu Waziri: Wahandishi wa maji wanyooke na asiyekubali kunyooka tutamnyoosha

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amewatahadharisha watumishi wote waliokuwa chini ya Tamisemi katika miradi ya maji ambao wamehamia Wizara ya Maji kwamba wanatakiwa kunyooka vinginevyo watanyooshwa.

“Nimshukuru sana Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa kutoa agizo la watumishi wote wa sekta ya maji kuwa chini ya Wizara yetu, nawatahadharisha kuwa lazima waje wakiwa wamenyooka na kama watashindwa sisi tutawanyoosha,’ amesema Aweso.

Aweso alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbarala, Haroon Mulla Pirmohamed bungeni leo Mei 14.

Pirmohamed alitaka kujua ni lini Serikali itamaliza kujenga skimu za umwagiliaji Ipatagwa, Kongoro/Mswiswi, Motombaya na skimu mpya ya Mhwela mpaka Kilambo.

Naibu Waziri amesema katika mwaka wa fedha 2017/18, Serikali kupitia halmashauri ya Mbarali ilitumia kiasi cha Sh 20 Milioni kwa ajili ya kufanya ukarabati mdogo wa banio la Igumbilo lililopo Kata ya Chimala ili kuwawezesha wakulima kuendelea kutumia banio hilo kwa shughuli za umwagiliaji kwa muda.

No comments:

Post a Comment