Serikali imesema kuwa mwanafunzi aliyemaliza shule binafsi inachukuliwa moja kwa moja kuwa anauwezo wa kulipa ada ya chuo kikuu hivyo wanafunzi wasiona na uwezo watapewa vipaumbele.
Hayo yameelezwa leo,Mei 21 Bungeni, Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Ole Nasha ambapo amesema kuwa bajeti ya mikopo kwaajili ya wanafunzi wanaoenda vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka ni sh. Bilioni 427.
“Kuhusu wasiwasi wa wazazi kwa wanafunzi ambao wamesoma kwenye shule za binafsi kupata mikopo ya kwenda katika elimu ya juu naomba niendelee kuweka wazi jambo ambalo tumekuwa tukizungumza, bajeti ya mikopo kwaajili ya wanafunzi wanaoenda vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka ni sh. bilioni 427 wakati wanafunzi ambao tunategemea kuomba kwa mwaka ni kama elfu 70 mwaka huu wa fedha unaoisha tuliweza kuwachuku wanafunzi elfu 30 na kwa mwaka unaokuja tunategemea idadi hiyo kufikia wanafunzi elfu 40,” amesema Nasha.
Ameongeza kuwa “Katika hali ambayo fedha iliyopo inaweza kuwachukua wanafunzi kiasi fulani ni lazima tufanye uchaguzi, uchaguzi wetu utaangali uwezo wa wazazi kulipa kwahiyo mwanafunzi aliyemaliza shule binafsi aliyesoma katika shule binafsi inachukuliwa moja kwa moja kuwa anauwezo wa kulipa chuo kikuu, mfano shule nyingi za binafsi ada inafika kuna zingine zinafika mpaka milioni 30 na nyingine unaweza kuta za chini kabisa milioni 1 na laki 5, kwahiyo tunachoomba wale watoto ambao hawana uwezo kabisa tuwape nafasi kwanza kabla hatujawachukua wale ambao historia yao inaonyesha wanauwezo wa kulipa. 
Hata hivyo kama itadhihirika kama kuna mwanafunzi ambaye alipata msaada wa kulipiwa shule binafsi tunahitaji tu ushahidi naye atapata ufadhili.”
Share To:

msumbanews

Post A Comment: