Tuesday, 29 May 2018

Mugabe Hatarini Kutumikia Kifungo

Bunge la Zimbabwe limesema aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe, huenda akatumikia kifungo gerezani iwapo atashindwa kuwasilisha taaarifa rasmi mbele ya kamati ya bunge inayochunguza shutuma za ufujaji wa dola bilioni 15 za ushuru uliotoka kwa mauzo ya Almasi.
Mwenyekiti wa kamati ya madini Temba Mliswa, amesema kuwa uvumilivu wa wabunge ulikuwa umefika mwisho, Baada ya kumsubiri rais huyo wa zamani kwa Zaidi ya nusu saa bila kufika mbele ya kamati hiyo ya madini.
Msilwa alisema barua waliyomwandikia ambayo ni ya mwisho, ilikuwa kumbusha kwamba anatakiwa  kufika mbele ya kamati hiyo, na matumaini yalikuwa ni kwamba isingehitajika kuchukua hatua ya kumlazimisha rais huyo wa zamani kufika mbele ya kamati hiyo.
Hii ni mara ya pili kwa Mugabe, mwenye umri wa miaka 94, kukosa kufika mbele ya kamati hiyo ili kujibu maswali kuhusu shutuma za ufisadi katika seka ya madini aina ya almasi.
Mnamo mwaka wa 2016, Mugabe na Zimbabwe walipoteza dola bilioni 15 kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ufujaji katika sekata hiyo.
Madini ya almasi yaligunduliwa nchini Zimbabwe mnamo mwaka wa 2006 na kuleta matumaini kwamba uvumbuzi huo ungesaidia kuimarisha pakubwa uchumi wan nchi hiyo uliodorora sana.
Ingawa utawala wa Mugabe uliyashutumu makampuni ya kuchimba madini kwamba hayakueleza faida yaliyokuwa yakipata, shirika la Global Witness na mashirika mengine ya uangalizi wa ufisadi, yalieleza wasiwasi juu ya matumizi mabaya ya fedha katika sekta hiyo ya madini.
Global Witness ilizilaumu idara za usalama na washirika wa kisiasa wa Mugabe kuwa walipora na kuhamisha pesa kutoka kwa sekta ya uchimbaji almasi na kuuza mawe hayo yenye dhamani kubwa na kujifaidi na mapato yote yaliyotokana na mauzo ya bidhaa hiyo.

No comments:

Post a comment