Tuesday, 1 May 2018

Mtanzania apewa tuzo ya uongozi bora na chuo kikuu nchini Marekani

Mtanzania N’nyapule Madai amepewa tuzo ya uongozi bora katika kuhudumia watu wenye ulemavu na Chuo Kikuu cha Minnesota nchini Marekani .
Picha inayohusiana
N’nyapule Madai
N’nyapule Madai ambaye ni Kamishna mstaafu Msaidizi Ustawi wa Jamii, amepewa tuzo hiyo Aprili 25, 2018 kwenye hafla maalumu iliyofanyika chuoni hapo.
Tuzo hiyo inayofahamika kwa majina ya University of Minnesota Distinguished Leadership Award  (UMN Awards) imetolewa kwa kutambua mchango wa Mtanzania huyo wa kuwahudumia watu wenye ulemavu.
Hata hivyo, akieleza furaha yake baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Madai amewataka Watanzania kutowaficha watu wenye ulemavu kwani wanauwezo wa kubadilisha maisha yao kupitia nyanja mbalimbali za kiuchumi.
Soma taarifa hiyo HAPA .

No comments:

Post a Comment