Friday, 25 May 2018

MKWASA: WACHEZAJI WAKO TAYARI KUKIPIGA NA RUVU SHOOTINGKatibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema kikosi chao kipo tayari kukabiliana na Ruvu Shooting katika Uwanja wa Taifa leo.

Mkwasa amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo wa leo huku akieleza kuwa mechi itakuwa ngumu kutokana na Ruvu Shooting kuonesha kiwango kizuri katika mechi kadhaa ilizocheza hivi karibuni.

Yanga inangia dimbani ikipigania nafasi ya pili ili kuweza kuwa makamu bingwa wa ligi. hivyo inahitaji kushinda mchezo wa leo na ujao dhidi ya Azam FC ili kufanikiwa maadhimio hayo.

Aidha, Katibu huyo amewaomba wapenzi na mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi Uwanjani ili wakatoe hamasa kwa wachezaji.

Mkwasa amesema baada ya mechi hiyo wataanza maandalizi ya kukabiliana na Azam FC, mchezo ambao utakuwa wa kuhitimisha safari yao katika ligi msimu huu.

No comments:

Post a comment