Mkuu wa mkoa wa mwanza John Mongella amewaagiza walimu wakuu wa shule za msingi mkoani humo kuacha tabia ya kuvifungia kwenye makabati au stoo vitabu vilivyotolewa na taasisi ya elimu nchini, badala yake vitumike kuwaazimisha wanafunzi kwa utaratibu unaofaa, ili kuhakikisha lengo la serikali la uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi watatu linatimia.

Mongella ametoa agizo hilo wakati akipokea vitabu zaidi ya laki 5 vyenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni 251 vya shule za msingi kwa darasa ya kwanza, darasa la pili na darasa la tatu vya masomo ya kuandika, kusoma, afya na mazingira, michezo na sanaa, maarifa ya jamiio na kiingereza.


Afisa elimu wa mkoa wa mwanza mwalimu michael ligola, amesema serikali inatambua adha wanazopata walimu katika ufundishaji na ujifunzaji hasa kipindi hiki ambacho elimu inatolewa bila malipo na kusababisha ongezeko kubwa la wanafunzi madarasani.

Lengo la serikali ifikapo mwaka 2025 ni kuhakikisha kitabu kimoja kinatumiwa na mwanafunzi mmoja. Kabla ya serikali kukabidhi vitabu hivyo wanafunzi wa madarasa hayo, kitabu kimoja kilikuwa kinatumiwa na wanafunzi watano.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: