Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Yanga umesitisha mkutano mkuu wa klabu uliopangwa kufanyika Jumamosi ya Mei 5 2016.

Mkutano huo ulikuwa ni mahususi kwa ajili ya kuzungumzia ajenda mbalimbali za klabu ikiwemo suala la uendeshaji.

Inaelezwa sasa mkutano huo utapigwa kalenda na itabidi ufanyike tena siku nyingine mbeleni badala ya Jumamosi ambayo ilipangwa awali.

Wapenzi wengi na mashabiki wa Yanga walikuwa wanausubiria haswa wakiwa na hamu kubwa ya kuzungumzia ajenda inayohusiana na uendeshwaji wa mfumo mpya wa kisasa ndani ya klabu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: