Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga amewacharukia Azam TV akiwalaumu kutokutangaza kitendo cha Kelvin Yondani kutemewa mate wakati wa mchezo wa Yanga SC dhidi ya Singida United uliofanyika Uwanja wa Namfua.

Mkemi amehoji iweje Azam TV hawajatilia nguvu kutangaza tukio hilo huku akieleza kuwa wao na Simba baba  yao ni mmoja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mkemi amewauliza Azam TV kuwa Camera zao zilikuwa wapi wakati tukio hilo linafanyika? Ina maana hawakuliona hilo?

"Kujisaidia ajisaidie kuku tu, Haji Manara, TFF na Azam TV hii haikushabikiwa wala hamkuitangaza kwakuwa nyinyi na Simba baba yenu mmoja, Azam TV hii kamera zenu haikuona siyo?" aliandika Mkemi.

Hata hivyo, Mkemi ameweka clip ya Azam TV inayoonyesha Yondani akiwa na mate eneo la sikio lake, akimtuhumu Batambuze kumtemea.

Baadhi ya wachangiaji wamekuwa wakimhoji Mkemi kwa hatua yake hiyo kwamba vipi anawalaumu Azam TV huku akitumia video ya Azam TV kuonyesha Yondani ametemewa matema.

Wengine wamemuuliza Mkemi kwamba hajui masuala yanayohusu uandishi wakati aliwahi kuwa mtangazaji kwamba Azam TV kazi yao ni kunasa matukio na kama walilinasa la Yondani kutema naye kutuhumu kutemewa, wanastahili lawama ipi?

Kauli hiyo ya Mkemi imekuja kuafuatia tukio la beki Yondani lililo gumzo hivi sasa mitandaoni kumtemea mate mchezaji, Asante Kwasi, katika mchezo dhidi ya watani zao wa jadi Simba uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi Jumapili.

Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Application yetu ya Msumba News ili upate habari zetu kwa wepesi zaidi kama vile Magazeti kuliko ilivyo sasa.

Tumekurahisishia; 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: