Saturday, 12 May 2018

Milioni 279 zatolewa kwa vijana na akina mama

Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Mkoani Mara imetoa Kiasi cha Fedha Shilingi Millioni 279 kwa ajili ya kukopesha Vikundi vya Vijana  na Akina Mama kupitia asilimia Kumi zinazoktokana na Mapato ya Ndani.

Akiongea na Waandishi wa habari Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyamwaga Kupitia Chama cha Demokrasia na Maendekeo CHADEMA Moses Misiwa Yomam amesema kuwa tangu wamechaguliwa 2015 Fedha zimeongezeka kutoka Millioni 36 kufikika sasa Millioni 279.

Tulipoingia katika Halmshauri hii tulikuta wanatoa fedha kiasi cha Shilingi Millioni Thelathini na Sita kupitia asilimia Kumi na Vijana na akina Mama lakini tumesimamia na kubana Matumizi kutokana na kile tunachokipata na kufikia Millini Miambili sabini na Tisa.

Mwenyekiti amesema kuwa Mwaka wa Fedha 2016-2017 walitoa Millioni 200 na sasa wametoa 279 sawa na Ongezeko la Millioni 79 na watazidi kuongeza kadili Mapato yanavyokusanywa na Kusimamiwa Vyema.

Yomam amesisitiza Vijana na akina Mama kuunda Vikundi na kuvisajili pamoja na kuwa Miradi hai ili waweze kupewa Fedha hizo kwa lengo la kujikwamua Kiuchumi.

Hata hivyo Mwenyekiti akizungumzia Makusanyo amesemakuwa tangu Wamechaguliwa wamekuwa wakivuka Lengo kutokana na Makusanyo wa Ndani wanakasimia.

Adam Mutasingwa ni Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Tarime amesema kuwa 2014-2015 Mpaka 2017-2018 wamekuwa na Vikundi 289 huku akieleza Changamoto wanazokubana nazo na kutaja kuwa Vijana hawana Mwamko Mkubwa wa kuomba Fedha hizo kwa ajili ya kujikwamua Kiuchumi.

No comments:

Post a comment