Thursday, 17 May 2018

MICHUANO YA KURUGENZI CUP YAENDELEA KURINDIMA MJINI HAYDOM MKOANI MANYARA

X1
Waamuzi wa mashindano ya Kurugenzi CUP 2018 iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga wakishuhudia manahodha wa timu ya Makulusa FC Regi Gisimoy (kulia) na Samwel wa timu ya Airport FC wakitakiana heri ya mchezo ambapo walifungwa mabao 3-0.X2 
Kikosi cha timu ya Makulusa FC wakiomba dua kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya timu ya Airport FC ambapo walifungwa mabao 3-0 X3 
Wachezaji wa akiba wa timu ya Airport FC wakiwa benchi la ufundi huku wakiendelea furahi mchezo ambapo waliifungwa Makulusa Fc mabao 3-0 
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza uwanjani kufuatilia mashindano ya Kurugenzi Cup’18 ambapo timu ya Airport waliibuka na ushindi wa magoli 3-0 
X5 
Baadhi ya wachezaji wakiushuhudia mpambano wa soka ukiwa unaendelea kwa kasi baina ya timu za Airtport FC dhidi ya Makulusa FC hazipo pichani. 
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza uwanjani kufuatilia mashindano ya Kurugenzi Cup’18 ambapo timu ya Airport waliibuka na ushindi wa magoli 3-0 X7 
Mmoja wa wachezaji akigangwa na madaktari baada ya kuumia mguu katika mchezo huo.

Michuano ya Kurugenzi Cup 2018 iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Hudson Kamoga imeendelea kutimua vumbi kwa timu ya Airport SC kuifunga Makulusa FC mabao 3-0.

Katika mchezo huo uliofanyika jana kwenye uwanja wa shule ya msingi Haydom, hadi mapumziko timu ya Airport SC ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Abubakary Maina dakika ya nne kwa njia ya penati.

Kipindi cha pili timu ya Airport SC ilipata mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji hatari Emmanuel Mallo kwenye dakika ya 50 na ya 55. Kwenye mchezo mwingine timu ya Stand United timu ya Mlimani FC iliifunga bao 1-0 na kuiondoa kwenye michuano hiyo.

Fainali ya mashindano hayo iliyoshirikisha timu 10 inatarajiwa kufanyika jumapili ya wiki hii kwenye viwanja hivyo vya Haydom.

Katibu wa chama cha soka wilaya ya Mbulu (MBFA) Joseph Nicodemus alisema michuano hiyo itakuwa chachu kwa vipaji vipya vya wilaya hiyo kupiga hatua kwenye mchezo huo.

Nicodemus alisema anatarajia timu zitakazoshiriki michuano ya ligi daraja la tatu ngazi ya wilaya zitapata wachezaji kwenye michuano hiyo ya Kurugenzi Cup 2018.

No comments:

Post a comment