Friday, 11 May 2018

Mbosso aeleza ‘unyama’ wa WCB upande wa video

Mbosso na WCB
Muimbaji Mbosso kutoka label ya WCB, Mbosso amesema video za ngoma zake ambazo zinatoka kwa sasa alifanyika kipindi kirefu sana.
Mbosso ametolea mfano video yake ya ngoma ‘Picha Yake’ kwa kueleza ilishutiwa June 2017 nchini Afrika Kusini lakini ikaja kutoka April 05, 2018.
“Picha yake ilikuwa ni video yangu ya pili ku-shoot tangu niwe rasmi kama msanii wa WCB hapo sijatambulishwa lakini tayari nilikuwa ni msanii wa WCB, ” amesema Mbosso.
Ameeleza video yake ya kwanza ku-shoot ni ya wimbo Nimekuzoea iliyotoka February 09 , 2018. Mbosso ni msanii wa sita kusaini WCB baada ya Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen na Lava Lava.

No comments:

Post a Comment