Na Timothy Itembe, Tarime
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi, Tarime na Rorya limemtia nguvuni Mfanyabiashara wa duka la vifaa  vya pikipiki Kata ya Turwa wilayani hapa, Wankru Mariba (38) kwa kosa la kupatikana na mali za wizi.

Kamanda Mkoa wa Kipolisi, Tarime na Rorya, Henry Mwaibambe aliwaambia Waandishi wa Habari ofisini kwake kuwa mfanya biashara huyo alikamatwa na askari wake wakati wakifanya doria.

Mwaibambe alitaja pikipiki hizo kuwa ni pamoja na T 804 CHG aina ya sky mark Racer yenye chases namba B 21 NCF 06A11 na pikipiki aina ya Honda yenye chases namba 2910001204.

Nyingine ni pikipiki yenye namba za usajili MC 309 BPW aina ya Snulg yenye chases namba LBRSPJB 56 H9003324 na pikipiki yenye namba MC 196 BPA aina ya Sunlg yenye chases namba  LBRSPJB56C9010675.

Aidha Jeshi la Polisi linatoa wito kwa jamii kujiepusha na tabia ya kununua, kuuza au kumiliki pikipiki bila kuwa na nyaraka muhimu za mauziano kutoka polisi ama TRA ili kuepuka usumbufu wa kukamatiwa chombo kinapobainika kuwa hakina nyaraka halali za umiliki, alifafanua Mwaibambe.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: