Serikali nchini Burundi kupitia Baraza la taifa la Mawasiliano (Conseil National de la Communation- CNC) imeyapiga marufuku mashirika mawili ya kimataifa ya utangazaji ya BBC na VoA .
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza
Taarifa ya kufungiwa kwa mashirika hayo imetolewa leo Mei 04, 2018 na Rais wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo, Karenga Ramadhan ambapo imesema kuwa mashirika mwisho wa kurusha matangazo yao nchini Burundi ni Mei 07 mwaka huu.
Sababu za mashirika hayo kufungiwa ni kufanya mahojiano na watu walioiasi Burundi wanaoishi ughaibuni na kuyarusha nchini humo kitu ambacho ni kinyume na sheria za mawasiliano na ni uchochezi.
Sambamba na adhabu hiyo, vituo vingine vitatu vya redio RFI, Isanganiro na CCIB FM vimepigwa onyo kali huku gazeti Le Renouveau la nchini humo likifungiwa miezi mitatu.
Sababu za kufungiwa kwa gazeti hilo ni kuandika habari ya kuandika makala zenye uchochezi zilizolenga kuikosoa serikali ya Rais Pierre Nkurunziza.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: