Friday, 25 May 2018

MASAU BWIRE AWATAKA MASHABIKI YANGA KUTOENDA UWANJANI LEO


Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire, amewataka mashabiki wa Yanga walio na roho nyepesi kutoenda Uwanjani leo kwa ajili ya mchezo wa ligi.

Ruvu Shooting itakuwa mgeni dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza mechi ya kukamilisha ratiba ya Ligi.

Bwire amewataka mashabiki hao wenye roho nyepesi kusalia nyumbani ili kuepuka kudondoka chini na kuzimia huku akijgigamba kuwa ni lazima Yanga waachia alama tatu leo kwa kueleza kuwa wataipapasa.

"Pengine niwaombe tu kwamba kwa mashabiki wa Yanga walo na roho nyepesi wasithubutu kuja Uwanjani leo kwa maana dhahama watakayokutana nayo itawaumiza, tutawapapasa" amesema.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 10 kamili jioni ambapo utarushwa mbashara na kituo cha Azam TV.

No comments:

Post a comment