Tuesday, 29 May 2018

MARCEL AWAOMBA RADHI WANASIMBA KWA SABABU HII MOJA


Na George Mganga

Mshambuliaji aliyekuwa anaichezea Majimaji FC msimu uliomalizika, Marcel Kaheza, amewaomba radhi wapenzi na mashabiki wa Simba baada ya kuifunga timu hiyo bao kwenye mchezo wa jana wa ligi kuu.

Marcel alifunga bao hilo dhidi ya Simba walipokutana kuhitimisha safari ya msimu wa 2017/18 wa Ligi Kuu Bara katika mchezo uliofanyika Majimaji Stadium na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kaheza ameomba radhi kutokana na kufunga bao hilo baada kuthibitisha rasmi kuwa amejiunga Simba na tayari ameshasaini mkataba na mabingwa hao wa ligi msimu huu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Marcel ameandika ujumbe unaoeleza kuwa anawaomba radhi Wanasimba kwani mechi hiyo haikuwa na umuhimu kwao akieleza tayari ni mabingwa wapya.Mchezaji huyo huyo anayecheza nafasi ya ushambuliaji amefunga jumla ya mabao 14 akiwa na Majimaji ambapo msimu ujao atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba.

No comments:

Post a comment