Wednesday, 9 May 2018

MAKONDA AMTAKA MKANDARASI KUIRUDIA BARABARA KWA FEDHA ALIZOLIPWA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza jambo kabla ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba ya barabara zenye jumla ya TSh. 5,876,689,896.00 zitakazojenga  kwa kiwango cha lami zenye urefu wa km 4.7. 
Makonda, akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya barabara zenye  zenye urefu wa km 4.7. zinazotarajiwa kujengwa.

Baadhi ya wakandarasi waliohudhuria hafla ya utiaji saini huo.
Baadhi ya wakandarasi wakiendelea kufuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Makonda akizungumza katika hafla hiyo.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  amemtaka mkandarasi aliyejenga barabara ya Kijitonyama inayopita kituo cha Polisi cha Kijitonyama ’Polisi Mabatini’ kurudia kuijenga kwa fedha za mkataba alizokwishalipwa kutokana na barabara hiyo kujengwa chini ya kiwango na kupelekea lami iliyokuwa imewekwa kubanduka.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akishuhudia utiaji  saini kwa mikataba ya barabara yenye gharama ya  jumla ya TSh. 5,876,689,896.00 zitakazojenga barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa km 4.7 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Box Culvet’s, barabara za changarawe na uzibaji wa viraka vya lami kwa baadhi ya barabara za jijini Dar kama vile, Haile Selassie, Magomeni-Makuti na Mwananyamala-Kisiwani.

Katika hatua hiyo Makonda ametoa rai kwa wakandarasi ambao wamesaini mikataba hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika mikataba akisema kuwa hataweza kukubali kuona kazi zinafanyika chini ya kiwango ndani ya mkoa wake na akiwataka mameneja wa wakala wa barabara vijijini na mijini  (TARURA) kuwasimamia wakandarasi ili wajenge miundombinu hiyo kwa viwango

No comments:

Post a Comment