Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewapa siku 45 watendaji wa soko la kimataifa la feri kuhakikisha wanarekebisha miundombinu mibovu ambayo imekuwa kero kubwa kwa wafanyabiashara wa maeneo hayo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana na kuona shimo kubwa katika eneo hilo ambalo kwa tathmini ya mafundi wamesema inatakiwa shilingi milioni 36 ili kulikarabati huku makusanyo ya ushuru ya soko hilo yakiwa zaidi ya shilingi milioni 90 kwa mwezi hali iliyompelekea kuwaambia watendaji hao wajitathimini kama wanatosha kuongoza

"Hapa kuna uzembe uliopitiliza na ukiona uzembe kama huu katika vitu ambavyo vya msingi vinavyohusu maisha ya watu, milioni 36 kwa shimo miaka miwili na nusu halijazibwa huu ni uzembe na hii inaonesha hata katika makusanyo yenu ya mapato kuna wizi mkubwa, huwezi kuniambia mmeshindwa kuziba shimo kama hili kwa milioni 36", alisema Jafo.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko hilo wamelalamikia huduma mbovu zilizopo katika soko hilo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: