Monday, 7 May 2018

LIVERPOOL HATIHATI KUSHIRIKI LIGI YA MABINGWA ULAYA, YAKUBALI KICHAPO CHA BAO 1-0 KUTOKA CHELSEABao pekee lillofungwa na Olivier Groud katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool limeiweka Chelsea nyuma kwa alama tatu dhidi ya majogoo hao wa London.

Chelsea iliyokuwa mwenyeji katika Uwanja wake wa nyumbani, Stamford Bridge, ilijipatia bao hilo katika dakika ya 32 ya mchezo.

Matokeo hayo yanaiweka Liverpool kwenye hatihati ya kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao kutokana na kichapo cha mchezo huo.

Endapo Liverpool ikimaliza kwenye nafasi ya tano ya msimamo wa ligi, itakuwa imeondoka tiketi rasmi ya kushiriki UEFA Champions League, pengine labda ikitwaa taji la mashindano hayo msimu huu itafanikiwa kuendelea kusalia kwenye michuano hiyo.

Dawa pekee ya Liverpool pia kusalia UEFA Champions League ni kushinda mechi za ligi zilizozalia 

Msimamo wa Ligi Kuu England unaonesha Liverpool imekamata nafasi ya tatu ikiwa na alama 72 huku Chelsea ikishika namba 5 ikiwa na pointi 62.

No comments:

Post a Comment