Saturday, 26 May 2018

KISA PENATI, MASHABIKI YANGA WAMTUPIA LAWAMA MWAMUZI


Mashabiki baadhi wa klabu ya Yanga wamelalamikia bao la Ruvu Shooting lililofungwa na mchezaji Khamis Mcha mnamo dakika ya 30 ya kipindi cha kwanza kuwa halikuwa sahihi.

Mcha aliitumia adhabu ya penati hiyo vizuri na kuweza kusawazishia Ruvu Shooting iliyokuwa nyuma kwa bao 1-0 wakati huo baada ya beki wa Yanga, Abdallah Shaibu 'Ninja' kuushika mpira katika eneo la hatari.

Penati hiyo imewaibua juu mashabiki wa Yanga ambapo wengi wamesema haikuwa halali wakieleza kuwa mpira ulimfuata Ninja na si Ninja aliufuata kwenye eneo hilo la hatari.

Mashabiki hao wamemponda Mwamuzi aliyecheza mechi hiyo wakidai kuwa alikosa umakini mpaka akawapa Ruvu bao la upendeleo.

Mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2 na kuziwezesha timu zote mbili kugawana alama moja moja.

No comments:

Post a Comment