Friday, 18 May 2018

Kigogo wa ACT na wanachama 6 wajivua uanachama na kutimkia CCM

 

Aliyewahi kugombea ubunge katika Wilaya ya Tarime kupitia chama  cha ACT wazalendo ameamua kukihama chama hicho kwa kile  kilichodaiwa kuwa ni kuunga mkono serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Mh John pombe magufuli.


Akizungumza na waandishi wa habari katika  ukumbi wa CCM Wilayani tarime aliyekuwa mgombea wa ubunge wilayani hapo kupitia ACT Wazalendo Tarime mjini 2015 Deogratias Meck   amesema kuwa ameamua kuhamia CCM kwa kile  alichotaja kuwa ni kukubali kazi inayofanywa na serikali ya chama hicho.

Akipokelewa na mwenyekiti wa chama  hicho wilaya Mh Daudi  Ngicho amesema kuwa sasa  Tarime ni muda muafaka kwa wanatarime kutambua mazuri yanayofanywa na chama  hicho nakukiuunga mkono  kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kupata maendeleo ndani ya wilaya na Mkoa wa Mara  kiujumla.

Pia Ngicho amewaasa wanachama wapya waliohamia katika chama  hicho kuwa wazalendo na nchi yao nakutorubuniwa na wachache wasioitakia mema  nchi yao.

Wanachama waliohamia chama cha mapinduzi  wametajwa kuwa ni Joseph Antony mkurugenzi wa Mipango na uchaguzi CUF wilaya ya Tarime ,Angelina Joseph KATIBU wa Kata sabasaba ACT ,Abigael Chacha,Deborah Chacha,Agnes Japhet , Ibraham Juma  Sengamgoda KATIBU ACT wilaya Tarime ,Deogratias Meck  mwanachama na mgombea ubunge kupitia ACT wazalendo 2015 Tarime.

No comments:

Post a comment