KAMATI ya kutetea wanahabari nchini Kenya, imemuomba Rais Kenyatta asiusaini muswada wa sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2017 uliopitishwa na Bunge la nchi hiyo hivi karibuni.

Muswada huo umesheheni vifungu vinavyotoa adhabu kali kwa mtumiaji wa mtandao atakayebainika kusambaza habari/taarifa ya uongo ambapo mtumiaji wa mtandao atakayetiwa hatiani kwa makosa hayo atakabiliwa na kifungo kisichopungua miezi 12 jela au faini ya Shilingi za Kenya Milioni 5(sawa na shillingi za Kitanzania zaidi ya Milioni 113).

Watetezi hao pia wameukosoa muswada huo kuwa umejaa vifungu vinavyokandamiza uhuru wa kujieleza na uhuru wa habari.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: