Friday, 4 May 2018

John Heche afunguka hatorudi nyuma


Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA), John Heche amefunguka na kusema kufuatia kifo cha mdogo wake Suguta Chacha ambaye aliuwawa kwa kuchomwa kisu na askari polisi basi yeye hatorudi nyuma kupigania haki za watu ili haki na usawa katika taifa viweze kushamiri.

Heche amesema hayo leo Mei 4,2018  siku moja baada ya kupumzisha mdogo wake kwenye nyumba yake ya milele na kusema kuwa kifo cha mdogo wake huyo ambaye amekufa kinyama kinazidi kumpa nguvu na sababu ya kupigania haki.

"Pumzika kwa amani Suguta, kifo chako cha kinyama kinanipa sababu zaidi ya kuendelea kupigania. Utawala wa sheria haki na usawa katika taifa letu. Sitarudi nyuma nitapambana mstari wa mbele wakati wote kwa heshima yako na kwa heshima ya Watanzania wote wanaopenda kuona nchi yetu inaongozwa vizuri"

Aidha Heche aliwashukuru watu mbalimbali ambao waliweza kujitokeza kumpumzisha mdogo wake huyo kwenye nyumba yake ya milele na kusema kuwa wamewapa faraja sana

"Asanteni Watanzania wote na Wanatarime kwa jinsi ambavyo mmekua faraja kwa familia yetu katika kipindi hiki kigumu endeleeni kupiga kelele kukemea uovu huu unaozalisha chuki katika Taifa letu.Pumzika kwa Amani “Simba

No comments:

Post a Comment