Sunday, 27 May 2018

Jibu la Belle 9 iwapo ndoa inamkwamisha kimuziki

Msanii wa muziki Bongo, Bell 9 amefunguka iwapo kufunga kwake ndoa kuna mkwamisha kivyovyote katika muziki.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma mpya ‘Dada’ ameiambia FNL ya EATV kuwa hamna kitu kama hicho ila kuna mabadiliko katika maisha yake ukilinganisha na hapo awali.
“Kwa kusumbua sanaa hapana, lakini maisha binafsi inakuchukua kidogo,” amesema Belle 9.
“Kama kijana zaidi ni usiriazi na familia kwa sababu vitu vimebadilika, kabla ya kufanga kuna vitu nilikuwa sivifahamu sasa navifahamu,” amesisitiza.
Katika hatua nyingine amesema kuwa mwezi wa tisa anatarajia kutoa EP ambayo itakuwa na jumla ya nyimbo 9 ambapo hadi sasa nyimbo tatu tayari amesharekodi.

No comments:

Post a comment