Tuesday, 8 May 2018

Harmonize ataja list ya wanaume 12 waliotembea na Jacqueline Wolper

Msanii Harmonize kutokea WCB na aliyekuwa mpenzi wake Jacqueline Wolper, sasa drama tele licha ya kuachana na kila mmoja kuwa na maisha yake.
Harmonize na Wolper
Msanii Harmonize kutokea WCB na aliyekuwa mpenzi wake Jacqueline Wolper, sasa drama tele licha ya kuachana na kila mmoja kuwa na maisha yake.
Harmonize anaingia katika headlines mara baada ya kutaja orodha ya wanaume ambao wanadai walishatoka kimapenzi na Wolper.
Hii ni baada ya Wolper kudai kuwa mpenzi wa Harmonize kwa sasa, Sarah ni mlezi wa wana. Harmonize kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
harmonize_tz….!!! zinaitwa hasira za fundi chereheni mchaga…..!! sasa jamani #sarah wawatu na huyu dada nani ni mlezu wa wana…..??? #Kikosi (A)
1 Dallas
2 mkongo
3 Simba
4 makochali
5 G modo
6 Chidi mapenzi
7 Konde_ boy
8 Chazi baba
9 brown
10 Engene
11 Jux, hebu nisaidie kuwatag kikosi (B) na (C) wacha niende zangu Mwanza.
Baada ya muda mfupi Harmonize alifuta post hiyo, hata hivyo Muigizaji Shamsa Ford alikereka na kitendo hicho mara baada ya kuona jina la mumewe, Chidi Mapenzi likihusishwa.
“Harmonize nakuheshimu sana mdogo wangu wangu, please nisingependa kuona jina la mume wangu kwenye huo ujinga wenu, Chidi kwenu anaweza akawa mshikaji kwangu ni mume.Kulikuwa hakuna haja ya kuweka jina lake wakati unajua ana maisha mengine. Tushichukuliane poa,” aliandika Shamsa Ford.
Harmonize na Sarah
Tangu weekend iliyomalizika couple ya Harmonize na Sarah imekumbwa na drama zenye kuchukua headlines za uzito wake. Chanzo cha yote ni pale zilipoibuka taarifa zilizobadai mpenzi wa Harmonuze anatoka kimapenzi na Bodyguard wa Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: