Halmashauri ya Arusha inategemea kuadhimisha Siku ya Hedhi Duniani itakayofanyika siku ya Jumatau,  28.05.2018 kwenye viwanja vya shule ya sekondari Mukulat kata ya Lemanyata.
Akizungumzia siku hiyo Afisa Afya halmashauri ya Arusha, Issa Msumari amesema kuwa siku hiyo ni muhimu kwa wasichana na wanawake wote ili  kuwa na hedhi salama isiyo na kikwazo.  
Ameongeza kuwa mwanamke anatakiwa kuwa na hedhi isiyokuwa na maudhi yoyote na isiyomkwamisha mwanamke kufanya shughuli zake za kiuchumi na isiyomkwamisha msichana kwenye masoma.
Msumari amefafanua hedhi salama ni ile isiyokuwa na vikwazo wala maudhi ikiwemo michubuko, muwasho na maumivu pamoja na kupata maji safi, vifaa vya kujisitiri pamoja na eneo la kujisitiria.
 "Mwanamke anatakiwa kupata hedhi isiyokuwa na michubuko, isiyokuwa na miwasho wala isiyokuwa na maumivu yoyote"amesema Afisa Afya huyo.
Naye mratibu wa miradi kutoka shirika la WaterAid Tanzania, Upendo Mntambo amesema kuwa, umefika wakati wa jamii kuanzia ngazi ya kaya, serikali na  taasisi zisizo za serikali kushirikiana na kuhakikisha mwanamke anapata hedhi iliyo salama. 
Mntambo ameeleza kuwa hedhi salama inamzuia mwanamke kupata magonjwa ya kuambikuiza kwenye via vya uzazi lakini pia inamfanya mwanamke kufanya shughuli zake bila kikwazo chochote akiwa na uhuru na amani mbele ya jamii yake. 
Siku ya hedhi duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 28.05.2018 na kauli mbiu ya mwaka huu ni 'HAKUNA TENA KIKWAZO' ikimaanisha kuwa na hedhi huru isiyo na kikwazo chochote.
Wananchi wote wa kata ya Lemanyata na kata za jirani wanaombwa kuhudhuria maadhimisho hayo ili kuoata elimu na maarifa zaidi juu ya hedhi salama na usalama wa mwanamke wakati wa hedhi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: