Wednesday, 30 May 2018

Diamond anafanya kazi, sijui hata kama huwa analala – Master J

Producer Mkongwe wa muziki Bongo, Master J amesema kuwa mafanikio ya Diamond Platnumz katika muziki ni kutokana na juhudi zake.

Master J amesema ambao wanaweza kumshangaa mafanikio anayopata kwa sasa pengine ni wale waliomjua hivi karibuni.
“Kwa wale ambao wanamjua kwa undani wanajua kwamba hivi vitu havijaja kwa urahisi, ni mtu ambaye anafanya kazi, sijui hata kama huwa analala, ana juhudi na ana bidii sana, kwa hiyo haya matunda tunaona leo ni matokeo kujitoa kwa miaka mingi sana,” amesema.
“Kwa hiyo mimi ninavyoona sasa hivi anaanza kupata matunda kusema kweli nafurahi sana na ninamshukuru Mungu,” Master J ameiambia Wasafi TV.
Licha ya kufanya vizuri katika muziki wa Bongo Flava, Diamond ameingiza bidhaa zake sokoni ‘Chibu Perfume na Diamond Karanga’ na sasa amefungua Wasafi Media na hivi majuzi ameweka wazi kumiliki moja gari la kifahari.

No comments:

Post a Comment