Tuesday, 29 May 2018

Diamond Akana Kumpigia Magoti Zari ili Warudiane

Msanii wa bongo fleva maarufu  nchini , Diamond Platinumz kwa mara ya kwanza amefunguka na kuzungumzia swala lake la kuachana na Zari na kumuomba radhi mwanamama huyo ambapo taarifa za hapo awali ziliwahi kusema kuwa kwa sasa Diamond amekuwa akipiga safari nyingi za Afrika ya Kusini ili kuomba radhi  kwa mwanamke huyo.

Akizungumzia kuhusu vijembe vingi ambavyo diamond amekuwa akitupiwa na mwanamama huyo hasa vya hapa karibuni alipokuwa kenya, Diamond alisema ; "hayo ya kenya bwana tuachane nayo, mimi nadhani yameshapita naomba tuendelee na  haya yasasa itapendeza sana”

Hata hivyo, mwandishi hakuishia hapo ndipo alipoamua kumuuliza moja kwa moja kuhusu yeye kusafiri kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya kuomba radhi kwa zari huku akienda kwa siri mara kwa mara na diamond alijjibu kuwa safari zake za afrika ya kusini hazihusiani na mambo hayo.

"N kweli ninaenda na so mara moja au mara mbili nimekuwa ninaenda,nakwenda kule sio kwa ajili ya kumuomba msamaha , hapana ila ninakwenda kule kwa ajili ya kuona wanangu tu,haiwezekani niwe ninatuma pesa za matumizi tu alafu ninafka mpaka afrika ya kusini na nisiende kuwaona wanangu.

"Hao wanaosema kuwa sijui nimekuwa nikimuangukia nadhani yatakuwa ni maoni yao tu wala sio yangu, ni maneno yasiyokuwa na msingi, zari ni mama wa watoto wangu na itabaki kuwa hivyo."

No comments:

Post a comment