CHUO cha Uhasibu Arusha(AII)kinatarajia kuanzisha programu mpya nne za Uzamili kwa fani ambazo zitawawezesha wahitimu kukubalika kwa urahisi katika soko la ajira za moja kwa moja nchini.
 
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo Uhasibu Arusha Dk. Samwel Welema wakati anazungumza na wadau kutoka katika mashirika na kampuni mbalimbali za binafsi na Serikali katika warsha iliyofanyika kwenye Chuo hicho Kitivo cha Dar es Salaam.
Amefafanua kuanzishwa kwa program  hizo kitakiwezesha chuo hicho kujihakikishia kwamba kile kinachofundishwa kitaenda kutumika na kinauhitaji mkubwa kwenye soko la ajira.

Dk.Welema amezitaja programu hizo ni Master of Science and Investment(MScFI),Master in Business Administration(MBA), Master in Business Administration in Information Technology Management(MBA-ITM) na Master of Business Administration in Procurement and Supplies Management(MBA- PSM)

Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Masomo ya Uzamili chuoni hapo, Grace Temba amesema, michango na maoni mbalimbali waliyoipata kutoka kwa wadau wakitaka kuanzishwa kwa program hizo mpya na ndio sababu ya chuo hicho kuona haja ya kuanzisha program hizo.

"Kwa kipindi cha miaka mitatu...minne, tumeweza kuongeza kusomesha walimu wetu hadi kufikia 16 ambao wanadigrii na wapo tayari kutoa elimu kwa hatua ya Uzamili" amesema Temba.
Amesema, wamepata maoni kutoka kwa wawakilishi wa mashirika na kampuni mbali mbali na lengo kuu ni kuhakikisha  kile ambacho kinaenda kutumika kinamahitaji kwenye soko la ajira.
Ameongeza, wahitimu wengi wanamaliza wakiwa wanajua nadharia tu, lakini sasa chuo kitakuwa kinatoa mafunzo kwa vitendo ambapo wahitimu watakuwa na uwezo mkubwa ukiwemo kuandaa ripoti, kusaidia kampuni na kuchanganua masuala mbalimbali kwa manufaa ya kampuni.
WhatsApp%2BImage%2B2018-05-04%2Bat%2B13.54.38
 Kaimu Mkuu wa chuo cha Uhasibu cha Arusha, (AII),  Dk. Samwel Welema akizungumza na wadau kutoka mashirika na makampuni mbali mbali nchini, juu ya azma ya chuo hicho kuanzisha programu nne za uzamili, katika warsha iliyofanyika katika chuo hicho kitivo cha Dar es Salaam.
WhatsApp%2BImage%2B2018-05-04%2Bat%2B14.10.38
WhatsApp%2BImage%2B2018-05-04%2Bat%2B14.11.05
 Mhadhiri wa chuo cha Uhasibu Arusha Kitivo cha Dar es Salaam, Allan Msola akiwaelezea wadau kutoka mashirika na makampuni mbali mbali nchini juu ya  programu nne za uzamili zinazotarajiwa kuanzishwa na chuo hicho hivi karibuni hapa nchini, katika warsha iliyofanyika katika chuo hicho kitivo cha Dar es Salaam.
WhatsApp%2BImage%2B2018-05-04%2Bat%2B14.43.12
Wadau na washiriki kutoka kwenye makampuni na mashirika mbali mbali wakifuatilia kwa making warsha iliyotolewa na chuo cha Uhasibu Arusha (AII) juu ya namna program mpya za uzamili zinazotarajiwa kuanzishwa na chuo hicho zitakavyowanufaisha wahitimu na makampuni watakayoenda kufanyia kazi.
WhatsApp%2BImage%2B2018-05-04%2Bat%2B14.07.20
Mkuu wa Idara ya masomo ya Uzamili wa chuo cha Uhasibu Arusha(AII), Grace Temba,akifafanua juu namna Program mpya zinazotarajiwa kuanzishwa na chuo hicho zitakavyofanya kazi na kuwawezesha wahitimu kukubalika moja kwa moja kwenye soko la ajira ndani na nje ya nchi
Share To:

msumbanews

Post A Comment: