Friday, 4 May 2018

CCM Mara watoa tamko kuuawa Mdogo wake Heche


Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mara kimelaani madai ya askari polisi kumuua kwa kumchoma kisu Suguta Chacha ambaye ni ndugu wa mbunge wa Tarime vijijini (Chadema), John Heche.

Akizungumza leo Alhamisi Mei 3. 2018 mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye amesema haiwezekani raia anayekamatwa kwa tuhuma yoyote kufariki kwa kipigo au sababu yoyote isiyohusika na ugonjwa wa kawaida akiwa mikononi mwa polisi.

"Nikiwa kiongozi na rafiki wa familia nalaani kitendo kilichofanywa na askari aliyefanya tukio hili," amesema Kiboye alipotoa salaamu wakati wa ibada ya mazishi ya kijana huyo inayoendelea muda huu.

Amesema kwa nafasi yake ya uenyekiti wa mkoa, ataendelea kuwahimiza watendaji wa Serikali, vyombo na taasisi zake  kutekeleza wajibu na majukumu yao kwa weledi wakizingatia sheria, kanuni na taratibu.

No comments:

Post a Comment