Tuesday, 29 May 2018

Bwawa la Nyumba ya Mungu lafurika


MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mughwira, ametoa taarifa ya kurufika kwa Bwawa la Mungu na kusababisha mafuriko makubwa katika wilaya za Mwanga, Same na Moshi Vijijini tangu mwishoni mwa wiki iliyopita.


Hali hiyo ilitokana na maji katika bwawa hilo kujaa zaidi na kupita kipimo chake cha ujazo na kusababisha maji kumwagikia katika sehemu kubwa za jirani ambako ni mashambani na makazi ya watu.

Kiongozi huyo amewapongeza watu, kampuni na taasisi binafsi ambazo zimetoa msaada kwa watu waliofikwa na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Mapato mkoani Kilimanjaro waliotoa kilo 330 za mchele, 140 za maharage ambapo kampuni ya Bonite imetoa kilo 100 za mchele na 20 za maharage.

No comments:

Post a comment