Thursday, 10 May 2018

BREAKING NEWS: SUGU NA MASONGA WAACHIWA HURU GEREZANI


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Nyanda ya Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kutoka Gereza la Ruanda Jijini Mbeya walikokuwa wakitumikia kifungo cha miezi mitano baada ya kukutwa na hatia ya uchochezi.Wawili hao wamepokelewa Uraiani leo Mei 10, 2018 asubuhi na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho waliosafiri hadi Mbeya kwa ajili ya mapokezi hayo.

Sugu na Masonga walikutwa na hatia hiyo  Februari 26 mwaka huu katika Mahakama ya Mkoa wa Mbeya ambapo walihukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kila mmoja.

No comments:

Post a Comment