Friday, 18 May 2018

BILL NAS AFUNGUKIA TUZO YA ‘AKWILINA’


William Lyimo ‘Bill Nas’
IKIWA ni siku kadhaa zimepita tangu msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, William Lyimo ‘Bill Nas’ kutunukiwa Tuzo ya Heshima na uongozi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) baada ya kutokea kuuaga mwili wa mwanafunzi Akwilina Akwilini chuoni hapo, hatimaye amefunguka alivyoipokea.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bill Nas aliandika ujumbe uliosomeka; “Ahsanteni sana wasomi na uongozi mzima wa Chuo cha (NIT) Dar es Salaam Campus.” Showbiz Xtra ilimtafuta msanii huyo, akafunguka:
“Nilialikwa ila kwa bahati mbaya nilikuwa kazini, nilikuwa na shoo Kigoma kwa hiyo nilituma wawakilishi. Tuzo hii imenifariji, pia nimeona kitu nilichokifanya sio kidogo,” alisema Bill Nas.

Bill Nas ndiye msanii pekee aliyefika kumuaga Akwilina, aliyefariki kwa kupigwa risasi Februari 16, 2018 ambapo aliomboleza pamoja na wafiwa.

No comments:

Post a comment