Monday, 14 May 2018

Babu Seya na Mwanaye Wametaja Sababu za Kushindwa Kwenda Kwao Congo

Wasanii wa muziki wa dansi, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ wameshindwa kwenda nyumbani kwao Congo kwaajili ya shughuli za kimila.

Wawili hao baada ya kusamehewa kifungo chao mwishoni mwaka jana, waliahidi kwenda nyumbani kwao kwa ajili kutembelea kaburi la mama yao mzazi.

Babu Seya amedai hawawezi kwenda nyumbani kwao kwa sasa kwa kuwa bado hawajapata pesa.

“Unajua ukienda nyumbani unatakiwa kuwa na pesa, sisi bado tupo kwenye mihangaiko ya pesa, mambo yakitulia tutaenda,” alisema Babu Seya.

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewaomba wadau wa muziki kuidhamini show yake ya kurudi rasmi kwenye muziki baada ya misukosuko ya muda mrefu ya gerezani.

No comments:

Post a Comment